Loading...

SERIKALI YAAGIZA WATUMISHI WA NSSF WALIOTAJWA KATIKA RIPOTI YA CAG KUCHUKULIWA HATUA

Loading...
  • Bodi mpya NSSF yatakiwa kuchukua hatua kwa watumishi waliohusika na ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka
  • Ni Watumishi waliotajwa katika ripoti za CAG na PPRA
Serikali imeipa miezi miwili Bodi mpya ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuwachukulia hatua watumishi waliohusika katika ubadhirifu, upotevu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka ambao wametajwa katika ripoti mbili za ukaguzi.

Watumishi hao ni wale waliotajwa katika ripoti za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) za mwaka wa fedha 2016/17.

Miongoni mwa upungufu uliobainishwa na CAG katika ripoti yake ni mkopo wa Sh7 bilioni uliotolewa katika taasisi ambazo hazikutajwa majina.

Nayo ripoti ya PPRA baada ya ukaguzi imebainisha kuwepo kwa malipo yenye utata kwa taasisi tatu yanayofikia Sh483.44 milioni zilizolipwa kwa mkandarasi, lakini hakuna kazi iliyofanyika. Ripoti hiyo imezitaja taasisi zilizohusika kuwa ni NSSF, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.

Akizindua Bodi ya NSSF juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama aliiagiza kupitia ripoti hizo haraka na kutoa uamuzi.

“Eneo hili nisingependa mpoteze muda, mlianza kutembea mapema, nitashangaa kama hamtafika hapa mapema. Ni eneo muhimu na ningependa lifanyiwe kazi kwa haraka,” alisema Mhagama.

Alisema bodi hiyo inayo mamlaka ya udhibiti wa nidhamu ya watumishi na kuitaka kuondoa aibu ndani ya shirika kwa kumwajibisha mfanyakazi atakatebainika kutaka kuliharibu.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Ally Siwa alisema wanajua kuwa bodi iliyopita ilisitishwa kutokana na sababu maalumu na kwamba, wao hawatawaangusha wananchi.
Na Geofrey Okechi.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SERIKALI YAAGIZA WATUMISHI WA NSSF WALIOTAJWA KATIKA RIPOTI YA CAG KUCHUKULIWA HATUA SERIKALI YAAGIZA WATUMISHI WA NSSF WALIOTAJWA KATIKA RIPOTI YA CAG KUCHUKULIWA HATUA Reviewed by By News Reporter on 10/29/2018 12:02:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.