Loading...
- Zaidi ya mashabiki 3500 wa soka walifanyiwa utafiti kuhusu nguvu za kiume walizo nazo wapenzi wao kitandani
- La kushangaza mashabiki wa klabu ya Man United walipatikana kuwa wadhaifu sana kitandani
- Klabu ya Arsenal ilikuwa na asilimia kubwa ya wapenzi ambao walidai kuwa wao ndio mashababi ikifikia masuala ya kitandani
Utafiti uliofanywa hivi maajuzi umeonyesha kwamba mashabiki wa klabu ya Manchester United ni wadhaifu sana wanapokuwa kitandani na wapenzi wao.
Kulingana na taarifa za jarida la Daily Mail, zaidi ya mashabiki 3,500 walichaguliwa kuzungumzia suala hili na kwa kweli matokeo yalikuwa ya kustaajabisha.
Utafiti huo ulionyesha kwamba sio wachezaji wa Man United pekee waliokuwa waking'ang'ana kuwa mabingwa kitandani ila pia mashabiki wao walikuwa wakijaribu kila wawezalo kuibuka washindi.
Mashabiki wa klabu ya Arsenal walichaguliwa kuwa bora zaidi kitandani baada ya kupata asilimia 11% wakifuatiwa na mashabiki wa Leicester kwa asilimia 10%.
Akizungumzia suala hilo, Dean North, alisema kuwa utafiti huo uliangazia kuwachangamsha mashabiki pamoja na wachezaji.
"Huwa linakuwa jambo la busara sana tunapoangazia maisha ya kibinafsi ya mashabiki na ya wachezaji wetu, na kwa kweli matokeo huwa yanafurahisha sana,' North alisema.
Na Timoth Andrew.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MASHABIKI WA KLABU YA MAN UTD NI WACHOVU ZAIDI KITANDANI, UTAFITI WAONYESHA
Reviewed by By News Reporter
on
10/29/2018 12:28:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: