Loading...

TAIFA STARS YAITEMBEZEA CAPE VERDE KICHAPO TAKATIFU

Loading...
Mchezo wa Marudiano wa kufuzu michuano ya #AFCON kati ya Tanzania(Taifa Stars) dhidi ya Cape Verde umemalizika.

Stars imeibuka na ushindi wa goli 2-0, zilizofungwa na Saimon Msuva na Mbwana Samatta.

Tanzania iliyocheza michezo minne na kujikusanyia alama 5 inakamata nafasi ya pili kwenye kundi L, linaloongozwa na Uganda yenye alama 7 baada ya michezo mitatu.

Kwenye kundi hilo Cape Verde inashika nafasi ya 3 ikiwa na alama 4 baada ya michezo minne huku Lesotho ikiwa nafasi ya mwisho na alama 2 baada ya michezo mitatu.

Na Jafar Mussa.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAIFA STARS YAITEMBEZEA CAPE VERDE KICHAPO TAKATIFU TAIFA STARS YAITEMBEZEA CAPE VERDE KICHAPO TAKATIFU Reviewed by By News Reporter on 10/16/2018 10:22:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.