Loading...

UINGEREZA YAISHUKU URUSI KWA MASHAMBULIZI YA MTANDAO

Loading...
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Uingereza kupitia kituo chake cha kitaifa cha usalama mitandaoni (NCSC)  idara ya kijasusi ya Urusi inayojulikana kama (GRU)  ilitumia mtandao wa wadukuzi kusambaza  taarifa  ulimwenguni.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa NCSC  ina uhakika kwa kiwango cha juu kuwa GRU huenda ikawa inahusika  na mashambulizi kadhaa ya kimatandao ikiwa ni pamoja na yaliyofanywa dhidi ya chama cha Democratic nchini Marekani kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt amesema vitendo vya taasisi hiyo ya GRU havifai kwani  vinajaribu kuhujumu demokrasia na kuingilia chaguzi katika nchi nyingine.

Hunt ameongeza kuwa ujumbe wao pamoja na washirika wao uko wazi na kuwa watafichua na kujibu  jaribio lolote la taasisi hiyo ya GRU la kuhujumu uthabiti kimataifa.

Uingereza inaamini kuwa Urusi inahusika  na mashambulizi hayo ya kimtandao.
Na Musa Twaha.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UINGEREZA YAISHUKU URUSI KWA MASHAMBULIZI YA MTANDAO UINGEREZA YAISHUKU URUSI KWA MASHAMBULIZI YA MTANDAO Reviewed by By News Reporter on 10/05/2018 08:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.