Loading...

VIJANA WASHAURIWA KUTUMIA FURSA ZA MIKOPO KUWEKEZA

Loading...
Vijana wametakiwa kutumia fursa mbali mbali za mikopo na kwenda kuwekeza kwenye maeneo ya uwekezaji wa viwanda ili kwenda kutimiza azma ya Tanzania ya Viwanda.

Ushauri huo ulitolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boifasi, alipokuwa akizungumza Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM kwenye semina ya kuwawezesha vijana kutambua fursa za mikopo ili kujikwamua kiuchumi.

Alisema nchi kwa sasa ipo katika safari ya kuelekea Tanzania ya Viwanda na kwamba ni jukumu la vijana kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kufikia malengo ya uchumi wa viwanda.

Boisafi alisema kuwa zipo fursa mbalimbali za mikopo kwenye almashauri zote nchini kwa vijana na kwamba lengo ni kukuza uchumi wa vijana na taifa kwa ujumla.

Vijana mkajiongeze sasa hivi wasomi ni wengi nafasi za ajira ni chache katika taasisi za serikali na binafsi na wanahitajika ni wake wenye uzoefu wa hali ya juu. Hivyo msitegemee ajira za serkali tu muwe wabunifu, nendeni mkawekeze ili mkazalishe ajira mpya," alisema Boisafi.

Alisema kuwa serikali inawasomesha ili wakatengeneze fursa za kujiajiri ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria ya nchi na kuhakikisha wanalinda amani ya nchi na kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa.

"Tengenezeni fursa mpya mpya, usitegemee kwenda kuajiriwa mnasoma ili mpata ufahamu kuhusu masuala mbalimbali yatakayo wawezesha kujipatia kipato na kuongeza uchumi wa taifa," alisema Boisafi.

Alisema atakwenda kwenye halmashauri ili vijana wenye sifa za kupewa mikopo ya asilimia nne ya vijana, wapewe ili wakaanzishe biashara ndogo ndogo.

"Pia tutakwenda kuilekeza halmashauri kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo kama wamachinga, lengo ni kuhakikisha kwamba wafanyabiashara hao wanafanya biashara zao kwa amani," alisema.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Abdulrahim Hamad, alisema vijana wengi bado hawajawa na uelewa kuhusu fursa za mikopo ya asilimia nne iliyotengwa na halmashauri na kwamba elimu zaidi bado inahitajika.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
VIJANA WASHAURIWA KUTUMIA FURSA ZA MIKOPO KUWEKEZA VIJANA WASHAURIWA KUTUMIA FURSA ZA MIKOPO KUWEKEZA Reviewed by By News Reporter on 10/05/2018 11:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.