Loading...
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman, amepiga marufuku walimu kwenda harusini saa za kazi.
Aidha, amewataka walimu wakuu kutowaruhusu walimu wenye tabio hiyo kuondoka shuleni.
Amesema serikali haitasita kumchukulia hatua za kisheria mwalimu atakayeondoka shuleni saa za kazi na kwenda harusini kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za utumishi wa umma.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa maagizo hayo hayo wakati akizungumza na walimu wa Skuli ya Msingi Mjananza katika ziara yake ya kushtukiza kwa lengo la kuangalia mafanikio na changamoto zinazoikabili skuli hiyo.
"Kuanzia leo, ni marufuku mwalimu kwenda harusini saa za kazi, kama ni harusi waende baada ya saa za kazi nawaomba walimu wakuu kutotoa ruhusa za aina hii," alisisitiza.
Alisema kulio kikubwa cha shule ni uhaba wa walimu, hivyo kuwapo kwa walimu wanaokwenda harusini saa za kazi, kunachangia ukubwa wa tatizo hilo.
Mapema, Mwalimu Othman Said Hamad, alisema changamoto inayowakabili katika shule hiyo ni wimbi la walimu kuaga kwenda harusini hasa siku za ijumaa.
Kutokana na changamoto hii, ni bora serikali ikifanya siku ya ijumaa kuwa ni siku ya mapumziko, kwani jamii imetutenga sisi walimu kwamba hatushiriki katika matukio ya kijamii ikiwemo harusi," alieleza.
Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Hamad Omar Issa, alisema baadhi ya wazazi hawana mwamko wa kielimu kwa watoto wao hususan wa kike, jambo ambalo linawafanya wakatishe masomo na kulazimika kuolewa.
"Hapa wapo wanafunzi watatu wa darasa la sita wenye umri wa miaka 14, walitaka kuolewa lakini serikali ya wilaya iliingilia kati ya kufanikiwa kuwarejesha skuli wanafunzi wawili ambao kwa sasa wanaendelea na masomo na mmoja bado hajarejea skuli," alieleza.
Fatma Juma Nassor, Mwalimu anayejitolea kwa zaidi ya miaka miwili, analia na tatizo la ajira na kuomba kama zikitoka, ziangalie zaidi walimu wanaojitolea.
Ziara hizi za kushtukiza zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa, zimelenga kuongeza uwajibikaji kwa watendaji wa taasisi za serikali.

RC APIGA 'MARUFUKU' WALIMU KWENDA HARUSINI
Reviewed by By News Reporter
on
10/05/2018 12:14:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: