Loading...
Chama cha Walimu nchini Kenya KNUT, kimetangaza kuwa kutakuwa mgomo wa walimu nchini humo kuanzia tarehe 17 mwezi huu, iwapo Tume ya kuwaajiri Walimu haitaachanana sera ambazo chama hicho kinasema zinatekelezwa bila ya kuwepo mashauriano.
Katibu Mkuu wa chama hichi Wilson Sossion amesema, iwapo tume hiyo itaendelea na sera hizo ambazo ni pamoja na kuwahamisha Walimu wakuu, mgomo huo utaendelea hadi pale suluhu itakapopatikana.
Iwapo mgomo utafanyika, utaathiri mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne na darasa la nane, unaotarajiwa kuanza baadaye mwezi huu.
Katibu Mkuu wa KNUT, Wilson Sossion amesema TSC haijaahidi kuyashughulikia malalamiko wanayoibua. KNUT inaitaka TSC kuwapandisha vyeo walimu, kuistisha mpango wa kuwahamisha walimu unaoendelea, vile vile shughuli ya kutathimini utendakazi wao.
Mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu chama cha walimu nchini KNUT kiliahirisha mpango wake wa mgomo uliokuwa ulipangwa kuanza tarehe 1 Septemba wakati wakiendeleza mazungumzo na muajiri wao TSC.
Na Hamidu Juma.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WALIMU WATISHIA MGOMO OKTOBA 17 KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
10/09/2018 06:11:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: