Loading...
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka kuwa chama chake kiko katika mikakati ya kufanya mageuzi ya kiuongozi, kitaasisi na utendaji ili kukiimarisha zaidi.
Polepole amesema kuwa mageuzi yatajikita katika maeneo hayo matatu, kwani kila eneo lina vipengele vyake ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya chama.
Polepole amesema kuwa wanaangalia idadi ya watumishi na uwiano wa uzalishaji kama vinaendana, weredi na mahitaji ya rasilimali watu, kiwango cha elimu pamoja na taarifa za wote wanaopokea mshahara kwani amedai kuwa CCM ndio chama pekee chenye watendaji wenye mishahara.
"Tunafanya mageuzi ya CCM, katika nyanja za maendeleo kwakuwa chama ni taasisi, tutafanya mageuzi ya kiuongozi tutaeleza ni viongozi wa namna gani tunaowataka", amesema Polepole.
Polepole amesema kuwa CCM ndio chama kikubwa Afrika, na kina watumishi wilaya zote nchini hivyo, mageuzi hayo yatakuwa na msaada wa kupata taarifa sahihi za uhakiki wa watumishi wake ndani ya chama.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com

CCM KUSUKWA UPYA, "TUNAFANYA MAGEUZI YA CCM"
Reviewed by By News Reporter
on
10/09/2018 06:00:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: