Loading...

WANAFUNZI 20,000 WASITISHA KUHUDHURIA MASOMO BURUNDI

Loading...
Wanafunzi zaidi ya elfu 20 waliokuwa wanapatiwa chakula shuleni na shirika moja la Kijerumani lisilo kuwa la kiserikali katika mkoa wa Kirundo kaskazini mwa Burundi wameacha kuhudhuria masomo shuleni.

Ikiwa wanafunzi laki moja na nusu wa shule za msingi katika mkoa huo, walikuwa wanapatiwa msaada wa chakula kutoka shirika hilo, kwa kupata mlo shuleni ili wasiache shule baada ya kudhihirika kwamba familia zao zinakabiliwa na umaskini.

Inaangaziwa kuwa hiyo ni moja ya athari ya hatua ya serikali ya Burundi kusitisha shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs ) 130 tangu tarehe mosi Oktoba, kwa madai kuwa mashirika hayo ya hisani hayaheshimu sheria mpya inayoongoza shughuli za mashirika ya kimataifa ya kigeni.

Serikali ilitowa masharti kadha kwa mashirika hayo na kuyapa muda wa miezi mitatu ili yawe yamekwisha tekeleza masharti hayo ili yaweze kuendele kufanya kazi.

Baadhi ya masharti hayo, ni pamoja na mashirika hayo ya kigeni kuweka pesa zao zote za matumzi za kigeni kwenye benki kuu ya taifa na kuhakikisha usawa kati ya makabila muhimu ya Burundi wakati wa kuajiri wafanyakazi.
Na Yahaya Hussein.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAFUNZI 20,000 WASITISHA KUHUDHURIA MASOMO BURUNDI WANAFUNZI 20,000 WASITISHA KUHUDHURIA MASOMO BURUNDI Reviewed by By News Reporter on 10/19/2018 07:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.