Loading...

KAMPUNI ZA MO WAKANUSHA TAARIFA YA UZUSHI INAYOSAMBAA

Loading...
Uongozi wa makampuni ya 'MeTL' unaomilikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji umekanusha taarifa za uvumi juu ya kusitisha shughuli za uzalishaji kwenye makampuni yake kufuatia tukio la kupotea kwa mmiliki wake Alhamisi ya wiki iliyopita.

Taarifa za kusitishwa kwa uzalishaji wa makampuni hayo zilianza kusambaa hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, zikiinukuu uongozi wake juu ya azma yake ya kusitisha uzalishaji ifikapo Oktoba 20 mwaka huu.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, MeTL imeandika, “tunaendelea kusikitishwa na tukio lililomtokea Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni yetu, Mohammed Dewji. Pia tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa tarehe 20/10/2018 tutasimamisha shughuli za uzalishaji katika makampuni yetu siyo za kweli.”

Mohamed Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi ya wiki iliyopitana mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za kupatikana kwake licha ya Jeshi la Polisi kuwashikilia na kuwahoji watu 26.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KAMPUNI ZA MO WAKANUSHA TAARIFA YA UZUSHI INAYOSAMBAA KAMPUNI ZA MO WAKANUSHA TAARIFA YA UZUSHI INAYOSAMBAA Reviewed by By News Reporter on 10/19/2018 07:24:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.