Loading...
Daniel Odongo amepitia mengi sana baada ya kuzaliwa kipofu. Baada ya kuipata stori yake, utakuwa na sababu zaidi ya kushukuru kuhusu maumbile yako. Daniel Odongo maarufu kama rubani kipofu alikuwa akiona miaka 25 iliyopita kabla ya kuwa kipofu.
Katika mahojiano na mtandao mmoja wa habari wa nchini Kenya alisimulia haya: "Nilizaliwa Agosti 24, 1992 na kwa miaka mitatu ya kwanza nilikuwa mtoto wa kawaida. Siku moja baba yangu alinituma jikoni nikamletee kijiko. Nilikitafuta bila mafanikio. Nisingeweza kuona na hapo ndipo baba yangu alipogundua kuwa nilikuwa kipofu. Alimwambia mamangu kuwa hakuwa tayari kuishi na motto kipofu,’’ Odongo alisimulia.
Kulingana naye, alipitia changamoto nyingi ikiwemo kutelekezwa na kufurushwa nyumbani kwa kuwa kipofu.
"Mamangu alitengana na baba yangu kutokana na hali yangu na kwa hivyo alipoamua kurudi, ilimbidi kuniacha kwa nyanya yangu licha ya kuwa na watoto tisa,'' alisema.
Nyanya yangu alipoanza kuugua, nilichukuliwa na wafadhili wengine wa katoliki walionipeleka shuleni. Nilifanya mtihani wa KSCE na kupata alama ya B- na kujiunga na Chuo Kikuu," aliongezea.
Hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji na kupata kuona tena.
''Nilijiuga na Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako nilisomea Elimu na kufuzu kwa daraja la kwanza.
Nilirudi katika mtaa wa mabanda ya Mathare nilikoanza kazi ya kushona viatu licha ya kuwa na ndoto ya kuwa rubani,'' alisema.
''Nilipoambiwa kuwa nilipaswa kulipa Ksh 750,000 (TSh17Mil) kama malipo ya kwanza, moyo wangu uliisha. Hata hivyo nilijikakamua na kupata KSH 20,000 (Tsh4.6Mil),’’ Odongo alisimulia.
Hadi sasa, Odongo ameweza kuendesha ndege hadi Mombasa na kurudi Nairobi huku akiwa na imani kuwa siku moja ataweza kumuendesha Rais Uhuru.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

KUTANA NA DANIEL ODONGO, RUBANI KIPOFU
Reviewed by By News Reporter
on
10/19/2018 08:13:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: