WANAWAKE walio katika umri wa kati, wametajwa kuwa kundi linaloongoza kwa kuvimba macho kutokana na matumizi ya bidhaa mbalimbali za urembo kama vile wanja, kupaka rangi machoni na kubandika kope bandia.
Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Bernadetha Shilio, alisema hayo jana kwenye kilele cha Siku ya Afya ya Macho Duniani.
Dk. Shilio alisema matumizi ya bidhaa hizo kwenye macho ya binadamu, yanachangia kwa

Loading...
iasi kikubwa matatizo mbalimbali ya macho.
Alisema takwimu za mwaka jana katika hospitali mbalimbali nchini zinaonyesha kuwa kundi kubwa la wanawake walio katika umri wa kati, wanaongoza kwa matatizo ya macho kuvimba.
Kwa mujibu wa Dk. Shilio, matumizi ya vipodozi hivyo katika macho yanamuweka mtumiaji katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya macho kutokana na kemikali ambazo zimetumika katika utengenezaji wake.
Mtaalamu huyo alisema hadi jana taarifa kutoka mikoa tisa zilibainisha kuwa watu 5,000 wamefanyiwa uchunguzi na 200 wamefanyiwa upasuaji.
Na Janeth Jackson.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WANJA, KUPAKA RANGI MACHONI NA KUBANDIKA KOPE BANDIA NI HATARI
Reviewed by By News Reporter
on
10/12/2018 08:22:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: