TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani Mara, imewafikisha mahakamani watuhumiwa saba akiwamo raia wa kigeni wa mgodi wa North Mara Gold Mine ulio chini ya kampuni ya Acacia kwa kosa la rushwa ya Sh. bilioni 13.5.
Fedha hizo Sh. 11,348,781,535 na Dola za Marekani 925,222 (sawa na Sh. 2,116,850,177), zinadaiwa kutolewa kwa lengo la kuwezesha upendeleo katika uthamini na maamuzi mbalimbali ya vijiji dhidi ya mgodi.
Watuhumiwa hao walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi, Veronika Mgendi, wakikabiliwa na kesi tano tofauti zinazohusu makosa ya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwenye mgodi huo

Loading...
kinyume na kifungu 15 (1) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Waliofikishwa mahakamani ni watumishi wa umma ngazi ya uthamini, Adam Yusufu, Peter Mrema na Joseph Kleruu.
Wengine ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja, Tanzania Omtima, Diwani kata ya Kemambo, Bogomba Chichake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakunguru, Abel Nyakibaru na raia wa kigeni ambaye ni Mhasibu wa mgodi huo, Marten Vande Walt.
Akisoma hati ya mashtaka, Mwanasheria wa Takukuru, Leonard Swai, alidai kuwa watuhumiwa hao walikula njama za kutenda makosa hayo kati ya Januari 2016 hadi Mei 2018, kwa nyakati na siku tofauti.
Na John Kassim.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com

VIGOGO ACACIA MAHAKAMANI KWA RUSHWA YA BIL. 13.5/-
Reviewed by By News Reporter
on
10/12/2018 08:05:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: