Loading...
Serikali ya Zimbabwe inaazimia kuwapa chanjo ya kipindupindu watu wapatao milioni 1.4 ikishirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO.
Ugonjwa huo hatari umeenea nchini humo hususan katika vitongoji vyenye msongamano wa watu katika mji mkuu, Harare.
Kulingana na taarifa ya Shirika la Afya Ulimwenguni, ugonjwa huo tayari umeuwa watu 49 tangu uliporipuka mjini Harare mwanzoni mwa mwezi uliopita wa Septemba.
Shirika hilo limesema watu takriban 8,000 wanahofiwa kupata maambukizi ya ugonjwa huo.
Watu 4,000 walikufa kwa kipindupindu mwaka 2008 nchini Zimbabwe katika mripuko mbaya kabisa wa ugonjwa huo kuikumba nchi hiyo. Ugonjwa huo aghalabu huenea kupitia matumizi ya maji machafu.
Na Mwaka Shabani.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

ZIMBABWE KUWAPA WATU MILIONI 1.4 CHANJO YA KIPINDUPINDU
Reviewed by By News Reporter
on
10/05/2018 07:47:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: