Loading...

ZIMBABWE: UPINZANI WATAKA KUUNDWA KWA SERIKALI YA MPITO

Loading...
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa ametoa wito jana wa kuundwa serikali ya mpito kutatua hali mbaya ya kiuchumi na mzozo wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo.

Upungufu wa fedha za kigeni katika wiki za hivi karibuni umezusha mzozo mkubwa wa kiuchumi ambapo upatikanaji wa mafuta , chakula na madawa unapungua. 

Hatua ya kwanza ni kwa nchi hii kuingia katika njia ya mjadala wa kisiasa, amesema Chamisa mwenye umri wa miaka 40, kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change MDC, ambaye amedai kwamba ameshinda uchaguzi wa rais wa hapo Julai 30. 

Chamisa ambaye alishindwa na rais wa sasa Emmerson Mnangagwa , amesema amekutana na viongozi wa kidini ambao wanataka mjadala wa kisiasa kati ya upinzani na rais.
Na Geofrey Okechi.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ZIMBABWE: UPINZANI WATAKA KUUNDWA KWA SERIKALI YA MPITO ZIMBABWE: UPINZANI WATAKA KUUNDWA KWA SERIKALI YA MPITO Reviewed by By News Reporter on 10/24/2018 07:15:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.