Loading...

AFUENI BAADA YA UTAFITI KUPATA DAWA YA KUTIBU HIV/UKIMWI

Loading...
Matumaini mapya yameanza kuonekana katika juhudi za kutafuta tiba ya virusi vya HIV baada ya kampuni ya Israel, Zion Medical kutengeneza dawa inayoweza kuangamiza asilimia 99 seli mwilini zinazoathirika na virusi hivyo bila ya kuathiri seli zilizo salama.

Kulingana na kampuni hiyo, dawa hiyo kwa jina Gammora inaweza kuweka sampuni ya jeni kwenye DNA ya seli zilizoathirika.

Awamu ya kwanza ya uchunguzi huo wa majaribio ulihusisha wagonjwa tisa waliokuwa na virusi vya HIV. 

Utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 90 ya virusi hivyo kwenye miili ya wagonjwa walioshiriki zilipunguka kwa wiki nne za kwanza.

Awamu ya pili ya majaribio hayo uliimarishwa na wagonjwa kupewa dawa hiyo pamoja na dawa nyingine ya kuzuia makali ya virusi vya HIV, zoezi ambalo lilionyesha kupungua kwa virusi hivyo kwa hadi asilimia 99.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AFUENI BAADA YA UTAFITI KUPATA DAWA YA KUTIBU HIV/UKIMWI AFUENI BAADA YA UTAFITI KUPATA DAWA YA KUTIBU HIV/UKIMWI Reviewed by By News Reporter on 11/05/2018 06:44:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.