Loading...
Jumla ya wanafunzi sita wa kidato cha nne katika eneo la Ukambani wamejifungua leo Jumatatu, Novemba 5 saa chache kabla mtihani wa KCSE kuanza rasmi kote nchini Kenya.
Wanafunzi wawili wa eneo la Mwingi wanaufanya mtihani huo katika hospitali ya Mwingi Level Four vitandani vyao.
Akizungumza na jarida moja la habari la nchini humo, mkuu wa hospitali hiyo Henry Mumo alithibitisha kuwa mwanafunzi mmoja alijifungua kwa njia ya kawaida huku mwengine akisubiri kujifungua. Aidha alithibitisha kuwa alibarikiwa na mtoto wa kike.
Usalama umeimarishwa katika chumba wanakofanya mtihani wanafunzi hao wawili.
Pia, jarida hilo limebaini kuwa wanafunzi wengine watano katika kaunti za Makueni na Kitui wanafanya mtihani wao hospitalini baada ya kujifungua.
Wanafunzi hao ni wa shule za Mathuma, Envuza, Vinada na Ungatu.
Na Hussein Bwanji.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WANAFUNZI 6 WAJIFUNGUA MTIHANI WA MWISHO - KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
11/05/2018 07:11:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: