Loading...

WADAU WA KOROSHO WAZIDI KUPETA, VYAMA VYA USHIRIKA VYAFUFULIWA

Loading...
Naibu Waziri wa Kilimo Tanzania, Mary Mwanjelwa amesema takribani tani 360,000 za vifungashio, kamba na magunia zitakazotumika kwa ajili ya kuhifadhia zao la korosho tayari zimeshawasili hapa nchini. Mwanjelwa amesema hayo katika mkutano wa hadhara Mkuranga na kueleza kuwa serikali imejipanga kuboresha na kufufua upya ushirika ili kuhakikisha korosho zinanunuliwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika.

“Serikali imejipanga kufufua na kuboresha ushirika, lengo ni kuhakikisha korosho zinanunuliwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika”. Ameeleza Naibu Waziri Mwanjelwa.

Mwanjelwa ameongeza kuwa kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani, msimu uliopita korosho iliuzwa kwa Sh. 3,000 kwa kilo moja ambapo ameeleza kuwa bei ya korosho kwa msimu uliopita ilikuwa Sh. 3,000 hadi Sh. 4,000.

Naibu Waziri huyo amesema serikali ya awamu ya tano inawajali wadau wa kilimo hivyo inafanya jitihada zote kuhakikisha zao la korosho linawanufaisha. Aidha, Mwanjelwa amewataka maofisa ugani kwenda maeneo ya vijijini na kusikiliza kero zinazowakabili wakulima na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.
Na Barakah Zeberi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WADAU WA KOROSHO WAZIDI KUPETA, VYAMA VYA USHIRIKA VYAFUFULIWA WADAU WA KOROSHO WAZIDI KUPETA, VYAMA VYA USHIRIKA VYAFUFULIWA Reviewed by By News Reporter on 11/05/2018 07:41:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.