Loading...

MTIHANI WAMUUA MWANAFUNZI: KENYA

Loading...
Kenya. Mtahiniwa wa mtihani wa KCSE, kutoka katika shule moja kaunti ya Nyamira ameripotiwa kufariki baada ya kuzira alipomaliza kufanya mtihani wake wa kwanza wa somo la hisabatia. 

Keith Mong'are mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili ya Gesiaga alikuwa na ugonjwa wa moyo. 

"Mtoto wangu amekuwa akiugua ugonjwa wa moyo kwa miaka kadhaaa sasa,nimehuzunishwa na kifo chake ila siwezi mkosoa Mungu," Babake Keith aliambia wanahabari wa mtandao wa Nation. 

Keith alikimbizwa katika kituo cha afya cha Omboga ila alifariki kabla ya kuhudumiwa na madaktari. 

Mwili wake ulipelekwa katika hifadhi ya wafu ya hospitali ya Kinara. 

Haya yanajiri juma moja tu baada ya mwanafunzi mwingine wa shule ya upili ya Gaichanjiru kuzirai na kufariki alipokuwa akisakata densi na wanafunzi wenzake.
Na geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MTIHANI WAMUUA MWANAFUNZI: KENYA MTIHANI WAMUUA MWANAFUNZI: KENYA Reviewed by By News Reporter on 11/06/2018 06:17:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.