Loading...
Watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 26 wameokolewa, baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama katika Ziwa Victoria nchini Uganda.
Hata hivyo, kuna hofu kuwa idadi kubwa ya watu hawajaonekana kwa mujibu wa ripoti za polisi.
Aidha, haijafahamika, boti hiyo ilikuwa na abiria wangapi.
“Kikosi chetu cha uokozi, kimewaokoa watu 26 wakiwa hai. Zoezi hilo linaendelea,” amesema msemaji wa Polisi Emilian Kayima.
Haijafahamika, kilichosababisha kuzama kwa boti hiyo.
Miezi miwili iliyopita, watu zaidi ya 200 walipoteza maisha hapa nchini baada ya kuzama kwa Ferry katika kisiwa hicho, katika Ziwa hilo ambalo linamilikiwa na nchi za Afrika Mashariki ya Kenya, Uganda na Kenya.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

AJALI YA BOTI: WATU ZAIDI YA 30 WAPOTEZA MAISHA ZIWA VICTORIA NCHINI UGANDA
Reviewed by By News Reporter
on
11/25/2018 02:09:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: