Loading...

DIDIER DROGBA ASTAAFU KUCHEZA SOKA

Loading...
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa timu ya taifa ya soka ya Cote d'Ivoire Didier Drogba, amesema anastaafu kucheza soka, baada ya zaidi ya miaka 20 katika viwanja vya mchezo wa soka.

Drogba mwenye umri wa miaka 40, anastaafia katika klabu ya Phoenix Rising nchini Marekani.

Alianza kucheza ya kulipwa mwaka 1998 katika klabu ya Le Mans nchini Ufaransa, kabla ya kwenda katika klabu ya Guingamp na baadaye kwenda Marseille.

Hata hivyo, umaarufu wake ulifahamika sana katika klabu ya Chelsea nchini Uingereza, alikofunga mabao 164 katika mechi 341.

Aliichezea timu yake ya taifa kati ya mwaka 2002-2014 na kuichezea mechi 104 na kufunga magoli 65, rekodi ambayo bado anaishikilia.
NA Samwel Owino.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DIDIER DROGBA ASTAAFU KUCHEZA SOKA DIDIER DROGBA ASTAAFU KUCHEZA SOKA Reviewed by By News Reporter on 11/23/2018 04:50:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.