Loading...

MANJI ATANGAZA RASMI KUREJEA YANGA

Loading...
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuph Manji ametangaza kurejea kazini na bado yeye ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga. Kupitia barua yake iliyosomwa mbele ya wanachama katika makao makuu ya klabu hiyo leo inasema Manji amekubali kurejea Yanga na ataanza kazi January 2019.

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la klabu Yanga Kapteni George Mkuchika amesema Yussuf Manji amerejea katika nafasi yake baada ya kumuandikia burua ya kukubali ombi la Wanachama wa klabu hiyo kumtaka atengue uamuzi wake wa kujiuzulu

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kikao kilichoitishwa na Baraza hilo, Kapteni Mkuchika ameonyesha barua iliyoandikwa na Manji kuridhia kurejea katika nafasi ya Uwenyekiti wa Yanga.

Kapteni Mkuchika amesema Manji aliandika barua ya kujiuzulu lakini wanachama walilikataa ombi lake kupitia Mkutano halali wa klabu hiyo na kumuomba arejee katika nafasi yake.

Barua hiyo aliyoandika ni uthibitisho kuwa ameridhia maombi ya wanachama wa Yanga na sasa ni rasmi amerejea katika nafasi yake.

Kapteni Mkuchika amesema Manji ndio Mwenyekiti wa Yanga huku Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Thobas Langalanga aliyekuwa.
Na Marry Timoth.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MANJI ATANGAZA RASMI KUREJEA YANGA MANJI ATANGAZA RASMI KUREJEA YANGA Reviewed by By News Reporter on 11/12/2018 01:27:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.