Loading...
Ukifika HOSPITALI YA MUHIMBILI kuna wodi inaitwa Sewahaji. Unamjua Sewahaji alikuwa ni nani??
Sewa Haji Paroo ndio hasa alianzisha ujenzi wa hospitali ya Muhimbili. Alifika huku Tanganyika kupitia kisiwa cha Zanzibar akitokea katika mji wa Bhuj.
Sewahaji alikuwa ni mfanyabiashara, na alikuja Afrika Mashariki kutafta Maisha. Mwaka 1852 aliamua kufungua Duka la bidhaa mbalimbali kwenye visiwa vya Zanzibar.
Biashara ilikuwa kubwa zaidi, Hivyo mwaka 1860 alifungua Duka Lingine Kubwa
Bagamoyo, kisha akaamua kuweka Makazi yake.
Biashara zake ikawa kubwa mno, hivyo Sewahaji akawa ni mmoja kati ya matajiri wakubwa.
Alisaidia Watu wote bila kujali Rangi, Dini wala Kabila zao. Alinunua Majengo kadhaa na kuyafanya Makazi Watu wasiojiweza na wasio na makazi waliokimbilia mzizima.
Alijenga shule za msingi na Hospitali kadhaa katika Mji Wa Mzizima (Leo ni Dar es Salaam).
Alijenga Hospitali akaiita Sewahaji Hospital ikawa inatoa Huduma bure kwa walalahoi wa Mzizima.
Mnamo Februari, 1897 Sheikh Sewa Haji Paroo alifariki Dunia.
Ilikuwa ni Huzuni na Simanzi kubwa wakazi wa Bagamoyo na Mzizima.Aliependwa sana!
Baada ya Kifo chake, Wakoloni wakabadilisha Jina Kutoka "Sewahaji Hospital" na ikaitwa "Princess Magreth Hospital"
Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo ya Wodi inaitwa SEWA HAJI.
Na Francis Daudi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MJUE MWANZILISHI WA WODI YA SEWA HAJI YA MUHIMBILI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
11/18/2018 09:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: