Loading...

MAREKANI KUKUMBWA NA TATIZO LA AJIRA

Loading...
Wiki iliyopita Nchini Marekani idadi wa watu waliokuwa wamejisajili kwenye orodha ya  wanaohitaji mshaara wa kutokuwa na kazi ilikuwa ni 234,000. Kiwango ni kikubwa kabisa kupata kurekodiwa ndani ya miezi 6.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na wizara ya kazi ya nchi hiyo, kwa mara ya kwanza idadi ya waliojiandikisha kuhitaji mshaara wa wasiokuwa na kazi  katika wiki inayoishia Novemba 24 ukilinganisha na wiki iliyotangulia iliongezeka kwa watu 10,000 kufanya idadi kufikia 234,000.

Kuanzia mwezi Mei mpaka hivi sasa Idadi kubwa  ya walijisajili kutokuwa na kazi wanaosubiri soko la ajira ilikuwa ni 220,000. Kufikia wiki iliyopita wastani wa watu waliokuwa wakijiandikisha kuhitaji mshahara wa kutokuwa na kazi ilikuwa 4,750 hivyo kufanya idadi kufikia 223,250

Kufikia Novemba 17 jumla ya idadi waliojiandikisha kwenye orodha ya wanaohitaji mshahara wa wasiokuwa na kazi ilifikia milioni 1 laki saba na kumi elfu imefahamishwa.
Na Mary Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAREKANI KUKUMBWA NA TATIZO LA AJIRA MAREKANI KUKUMBWA NA TATIZO LA AJIRA Reviewed by By News Reporter on 11/30/2018 10:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.