Loading...

MSANII WEMA SEPETU AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU

Loading...
Msanii wa Filamu, Wema Sepetu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Slaam akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili. Inadawa ni kutokana na kusambaa mitandaoni kwa video zake za faragha.

Wema amefikishwa mahakamani hapo leo Alhamisi, Novemba 1, 2018,majira ya saa 4 asubuhi akiwa amevaa miwani na kujitanda ushungi kichwani huku akisindikizwa na askari wawili ambapo alipelekwa kwenye chumba cha mahabusu cha mahakama hiyo.

Jana taarifa zilisambaa mitandaoni kuwa msanii huyo ambaye ni mshindi wa Taji la Miss Tanzania Mwaka 2016, alikuwa amekamatwa na polisi lakini taarifa hizo hazikuthibitishwa.

Hivi karibuni msanii huyo alisambaza mitandaoni video zake za faragha akiwa na mpenzi wake, PCK. Licha ya kuomba radhi siku chache baadaye, Bodi ya Filamu nchini ilimfungia msanii huyo kujihusisha na masuala ya sanaa kwa muda usiyojulikana huku ikisema adhabu yake inakuja.
Na Ummy Kisanga.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MSANII WEMA SEPETU AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU MSANII WEMA SEPETU AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU Reviewed by By News Reporter on 11/01/2018 12:18:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.