Loading...

Zimbabwe: Polisi wavamia ofisi za nabii aliyedai anatiba ya virusi vya UKIMWI.

Loading...
Polisi nchini Zimbabwe wamevamia ofisi za kiongozi wa kidini ambaye alisema kuwa ameanzisha tiba ya VVU, UKIMWI na Kansa, gazeti la Herald limetaarifu.

Walter Magaya, ambaye ni mchungaji wa Huduma ya Utaalamu wa Uponyaji na Uokoaji, alisema siku ya jumapili kuwa mimea, inayoitwa aguma, inaweza kuharibu/kuua virusi vya UKIMWI.

Tangazo lake lilisababisha gumzo, gazeti la Herald lilisema.

"Ukiendelea kutumia aguna, utaanza kuona hesabu za CD4 zako kuacha mpaka virusi vinakwisha na kutokuwa na maambukizi," tovuti ya New Zimbabwe ilimnukuu akiuambia mkutano.

Waziri wa Habari na Nishati Mutodi alithibitisha uvamizi huo kupitia mtandao wa twitter akisema sampuli za aguma zilizuiliwa na kutangaza kwamba "hakuna tiba bado" kwa VVU.
Na Joseph Kabila.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
Zimbabwe: Polisi wavamia ofisi za nabii aliyedai anatiba ya virusi vya UKIMWI. Zimbabwe: Polisi wavamia ofisi za nabii aliyedai anatiba ya virusi vya UKIMWI. Reviewed by By News Reporter on 11/01/2018 04:37:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.