Loading...

MTANZANIA ACHAGULIWA KATIKA WANAWAKE BORA 100 WA BBC 2018

Loading...
BBC imetangaza orodha ya wanawake 100 bora wenye ushawishi kutoka kote duniani kwa mwaka 2018.

Katika orodha hiyo Mtanzania Julieth Sargeant, ameshikilia nafasi ya 53 kama mbunifu wa kupamba bustani.

Juliet ni daktari, ambaye kwa sasa anajihusisha na kutengeneza bustani ili watu 'wahisi vizuri wanapozitembelea kama kwa mfano wa uzuri unaoonekana'.

Alitunzwa kwa kulipangia bustani iliyodhihirisha na kuhamasisha kuhusu utumwa mambo leo.

Bustani hiyo ilijumuisha milango kadhaa na mti wa Mwaloni - iliyodhihirisha kukamatwa, na mti ambao William Wilberforce alikaa chini alipo apa kusaidia kumaliza biashara ya utumwa.

Bustani hiyo ilibuniwa kuadhimisha siku ambayo bunge Uingereza lilipitisha sheria ya 2015 ya kupambana na utumwa wa mambo leo.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MTANZANIA ACHAGULIWA KATIKA WANAWAKE BORA 100 WA BBC 2018 MTANZANIA ACHAGULIWA KATIKA WANAWAKE BORA 100 WA BBC 2018 Reviewed by By News Reporter on 11/20/2018 10:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.