Loading...

MUHIMBILI SASA KUFANYA UPASUAJI WA TAYA NA FUVU

Loading...
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imefanya upasuaji mkubwa wa aina yake wa kuunganisha mifupa ya fuvu na kutengeneza taya kwa wagonjwa tisa.

Upasuaji huo unagharimu Sh. milioni saba kwa mgonjwa mmoja akitibiwa hapa nchini, wakati nje ya nchi ungegharimu zaidi ya Sh. milioni 60.

Daktari bingwa wa upasuaji wa taya, kinywa na uso kutoka Hospitali ya MNH, Daud Shabani, aliwaambia waandishi wa habari jana wakati wakifanya upasuaji huo.

Alisema walianzisha kambi maalum kwa ajili ya kufanya upasuaji huo unaochukua saa saba baada ya kupata wageni kutoka Hospitali ya Kansas City na Chuo Kikuu cha Missouri, Marekani.

Alisema wataalamu hao walikuja kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi, utaalamu pamoja na kuwapatia msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh. milioni 250 ambavyo vitawasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo hayo.

Aidha, Dk. Shaban alisema wataendelea kufanya upasuaji huo hata kama wataalamu hao wataondoka kwa kuwa vifaa wamepatiwa na wataalamu wako 13 wenye uzoefu katika ugonjwa huo.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MUHIMBILI SASA KUFANYA UPASUAJI WA TAYA NA FUVU MUHIMBILI SASA KUFANYA UPASUAJI WA TAYA NA FUVU Reviewed by By News Reporter on 11/23/2018 07:44:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.