Loading...

MUIGIZAJI FAIZA ASEMA MAKALIO SIO DILI, WADADA MJIKUBALI

Loading...
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu kwenye mitandao ya kijamii Faiza Ally amejikuta akiwatolea Povu Zito wanawake ambao wamekuwa wakimsumbua kuhusu madawa ya kuongeza makalio.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliweka wazi kuwa kuna wanawake wamekuwa wakimsumbua kwa kutaka kumtuma madawa ya kichina ya kuongeza makalio.

Faiza alisema hakuna jambo ambalo halipendi kama mtu kumuagiza dawa za kufanya mabadiliko kwenye mwili hivyo anawasihi wanawake wajikubali kama walivyoumbwa.

"Sipendi wanawake kutojikubali. Mimi siwezi kumletea mtu dawa ya kuongeza makalio maana naona kama si za kweli, lakini pia ni vyema kujikubali, hicho ndicho kitu muhimu".

Faiza ambaye hivi sasa yupo China kwa ajili ya kufunga mizigo ya wateja alianika meseji za wanawake ambao wanaomba kuletewa madawa ya kuomgeza hipsi na makalio.
Na Catherine Joseph.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MUIGIZAJI FAIZA ASEMA MAKALIO SIO DILI, WADADA MJIKUBALI MUIGIZAJI FAIZA ASEMA MAKALIO SIO DILI, WADADA MJIKUBALI Reviewed by By News Reporter on 11/12/2018 09:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.