Loading...
Wakazi wa kijiji cha Magumu, kaunti ya Nyandarua nchini Kenya walibaki kwa mshangao mkubwa baada ya jamaa wao kujitokeza siku mbili baada ya kuzikwa.
Wakazi walitoka mbio baada ya kumuona jamaa huyo akiingia nyumbani kwake alikozikwa awali.
Kulingana na familia yake, Paul Gicheche mwenye umri wa miaka 21 aliyekuwa akifanya kazi ya kuchunga ngombe alitoweka Septemba, mwaka huu.
Familia yake ilimtafuta bila mafanikio kwa muda hadi walipopata habari kuwa miili miwili ilipatikana katika msitu wa Ngumbi.
Waliamua kuuchukua mwili huo na baada ya kufanyiwa upasuaji wa maiti, waulizika wakiamini ni mwanao aliyepotea.
La kushangaza ni kuwa Gicheche aliyedaiwa kufariki na kizikwa alionekana tena siku mbili badaye.
Gicheche pia alishikwa na mshangao alipowaona watu wakimkimbia.
"Nilishangaa nilipofika katika soko la nyumbani, nilimuona rafiki yangu mmoja akinikimbia. Nilienda Longonot na singeweza kupata redio, runinga ama hata simu katika boma nilipokuwa nikifanya kazi, Nilifika hapa na kushangaa kupata habari kuwa nilikufa na kuzikwa," Gicheche alisema.
Naibu kamishna wa kaunti ya Kinangop Peter Nyameti aliyethibitisha kisa hicho alieleza kuwa uchunguzi zaidi ungeendelea kuhusiana na kisa hicho.
Na Husna Ramadhani.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

JAMAA AIBUKIA MTAANI BAADA YA KUZIKWA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
11/10/2018 10:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: