Loading...

MWANAMKE AVUA NGUO MBELE YA RAIS KULAANI UBAKAJI

Loading...
Phindile Ncube alikuwa akiongea kwenye kongamano la vita na mauaji ya kinyumbani lililojumuisha mashirika ya kutetea haki za binadamu, madaktari wa kienyeji na mashirika ya kidini.

Ncube alisema alilazimika kufanyiwa upasuaji wa tumbo mara tano; mojawapo ya upasuaji ukifanywa kutoa plastiki iliyokuwa imesokomezwa ndani ya uke wake wakati wa ubakaji huo. 

Ncube akiwa analengwa lengwa na machozi alisimulia uchungu wa kuwaona waliombaka wakiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne.

Alifunua rinda lake jeusi, akiwaacha waliohudhuria kongamano- akiwemo Rais Cyril Ramaphosa- kujionea makovu hayo. 

"Hatuwezi kuishi kama wafungwa, mheshimiwa Rais; kifungo cha chini kabisa kwa wabakaji kinafaa kuwa miaka 50," alisema Ncube.

Akihutubia kongamano hilo, Rais Ramaphosa alisema kuwa serikali yake itafanya kila juhudi kupunguza idadi ya visa vya ubakaji nchini humo.

"Hatutapumzika hadi tutakapomaliza visa hivi na kuafikia takwimu za sifuri," alisema Ramaphosa.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MWANAMKE AVUA NGUO MBELE YA RAIS KULAANI UBAKAJI MWANAMKE AVUA NGUO MBELE YA RAIS KULAANI UBAKAJI Reviewed by By News Reporter on 11/08/2018 10:36:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.