Loading...

MWANAMKE MMOJA AMUUA MWANAYE KISA MAEMBE YA JIRANI

Loading...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye RAHEL MATALAKA, miaka 41, mkazi wa kijiji cha lugenge, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake wa kiume aitwaye MALIATABU CONSTANTINE, miaka 10, mwanafunza wa darasa la pili shule ya msingi Ikelege.

Tukio hilo la mauaji limetokea tarehe 03.11.2018 majira ya 1:00 usiku, hii ni baada ya mama wa marehemu kuletewa malalamiko kuwa mtoto wake alikua akiangusha na kuiba maembe kwa jirani. Ndipo mtuhumiwa alipatwa na hasira na kumpiga mtoto kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyopelekea mtoto kupoteza fahamu na baadae kufariki dunia.

Mtuhumiwa alipoona mtoto amepoteza maisha alimchukua na kumtundika juu ya mwembe kwa kutumia kipande cha khanga ili apoteze ushahidi ili baadae ionekane kuwa amejinyonga. Ndipo majirani walipoona tukio hilo walitoa taarifa kituo cha Polisi.  Aidha baada ya polisi kupata taarifa hizo tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Polisi wamesema, wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa  ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Na Timoth Rashid.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MWANAMKE MMOJA AMUUA MWANAYE KISA MAEMBE YA JIRANI MWANAMKE MMOJA AMUUA MWANAYE KISA MAEMBE YA JIRANI Reviewed by By News Reporter on 11/07/2018 05:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.