Loading...
NDEGE mbili mpya aina ya Airbus 220-300 zilizotegemewa kuwasili nchini mwezi huu, sasa zitawasili mwezi ujao huku Boeing 787-8 Dreamliner nayo ikitegemewa kuanza safari zake India mwezi huo.
Ndege hizo zina uwezo wa kubeba abiria 132, abiria 12 wa daraja la kwanza na 120 daraja la kawaida. Awali, ndege hizo zilijulikana kwa jina la Bombardier C Series, na Julai mwaka huu Kampuni ya Airbus inaozitengeneza iliingia mkataba wa ununuzi na kuzibadilisha jina na sasa zinaitwa A220-100/300.
Zote zimenunuliwa kwa fedha za Serikali ya Tanzania ikiwa ni juhudi za Rais John Magufuli za kufufua shirika hilo la umma la ndege ili kuwezesha nchi kuwa na ndege zake na hivyo kuchangia zaidi katika pato la Taifa kupitia utalii kwa kuingiza watalii wengi nchini wanaosafiri moja kwa moja kuja nchini.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

NDEGE YA AIRBUS ATCL ZITAKAZOWASILI DISEMBA
Reviewed by By News Reporter
on
11/03/2018 07:15:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: