Loading...

MAMBO MUHIMU KATIKA KUFANIKISHA MALENGO YAKO

Loading...
Moja, Kufanikisha malengo yako inahitaji kufanya kazi kwa nguvu na bidii muda wote bila kupoteza hamasa na imani ya kufikia kusudi ulilojiwekea.

Pili, Kufanikisha malengo yako ni lazima uwe tayari kuheshimu na kujali muda wako na kutumia muda huo kwa ajili ya kufanikisha kusudi ulilojiwekea, kuepuka matumizi ya muda kwa mambo ambayo si ya msingi na ambayo hayakusaidii kufanikisha malengo yako.

Tatu, Kufanikisha malengo yako ni lazima ujenge uwezo wa kuheshimu na kuwa na nidhamu juu ya matumizi ya kila fedha unayoipata, matumizi yako yalenge katika kufanikisha malengo uliyojiwekea.

Mwisho, Kufanikisha baadhi ya malengo itakulazimu kuwa tayari kuachana na baadhi ya marafiki na watu ambao wako kinyume na kusudi unalotaka kufanikisha, kubadili aina ya watu unaokutana nao mara kwa mara na kuanzisha urafiki mpya na watu ambao wako tayari kukusaidia kufikia kusudi ulilojiwekea.

Keep Moving Forward!
Vicent Stephen



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAMBO MUHIMU KATIKA KUFANIKISHA MALENGO YAKO MAMBO MUHIMU KATIKA KUFANIKISHA MALENGO YAKO Reviewed by By News Reporter on 11/04/2018 11:53:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.