Loading...

AUNTY EZEKIEL AJITAPA KWA UHODARI SEKTA YA MAHABA

Loading...
MWIGIZAJI na staa wa filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel amesema kuwa ana sifa ya uhodari kwenye mapenzi na ndio maana akiingia sehemu huwa anaondoa wote waliokuwepo na kubaki yeye.  

Katika mahojiano na gazeti moja la udaku, Aunty alisema kuwa linapokuja suala l a kumpenda mtu hata akiwa na nani atamuachia tu kwani anajijua ni hodari wa kuondoa wote waliokuwa kwenye himaya hiyo.

“Siwezi kuanika moja kwa moja ninafanya nini na kwa nini wakiwa kwangu hawafurukuti, lakini najua wazi kuwa nina sifa hiyo na sijawahi kushindwa kwenye hilo,” alisema Aunt.

Aunty ambaye kwa sasa anapika na kupakua na Moze Iyobo, amepita kwa wanaume mbalimbali wakiwemo Hartmann Mbilinyi na Sunday Demonte ambao wote walikuwa wana watu wao lakini alipowanasa, aliwatuliza, wakawa hawafurukuti kwake.
Na Hamisi Makungu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AUNTY EZEKIEL AJITAPA KWA UHODARI SEKTA YA MAHABA AUNTY EZEKIEL AJITAPA KWA UHODARI SEKTA YA MAHABA Reviewed by By News Reporter on 11/04/2018 03:43:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.