Loading...

NDOA YA LULU YANUKIA, ATOLEWA MAHARI

Loading...
BAADA ya Staa wa Filamu BONGO, ‘Elizabeth Michael’ maarufu kama Lulu kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Majizzo, usiku wa Septemba 30, mwaka huu, hatimaye wawili hao wamepiga hatua nyingine kuelekea kwenye ndoa yao.

Jana Jumapili, Novemba 18, 2018, Majizzo alimtolea mahari mrembo huyo ikiwa ni takribani siku tano tu baada ya kumaliza kifongo chake alichkokuwa akikitumikia kwa kosa la kumuua mwigizaji Steven Kanumba bila kukusudia.

Katika ukurasa wake wa Instagram, baada ya kumaliza kutoa mahari kwa familia ya Lulu, Majizzo ambaye pia ni mwanzilishi wa Radio EFM na TVE aliandika; “Deal Done” huku Lulu kupitia akaunti yake ya Instagram naye akiweka picha na Emoji yenye ishara ya mtu akifanya maombi na kumshukuru Mungu.

Mastaa kibao walikuwepo kuhudhuria sherehe hiyo ya kutolewa mahali kwa Lulu jambo ambalo ni hatua mpya kuelekea ndoa yao inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Na Mary Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NDOA YA LULU YANUKIA, ATOLEWA MAHARI NDOA YA LULU YANUKIA, ATOLEWA MAHARI Reviewed by By News Reporter on 11/19/2018 04:12:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.