Loading...
Baraza la Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC), limekifungia kiwanda cha kusindika nyama ya punda kilichopo kwenye Jiji la Dodoma, baada ya ukaidi wa muda mrefu wa mmiliki kufuata taratibu sahihi za uhifadhi wa mazingira.
Kiwanda hicho ambacho kinamilikiwa na kampuni inayofahamika kama Huwachen Company Limited, kimekuwa kwenye mvutano wa muda mrefu na Baraza pamoja na Wizara inayohusika na uhifadhi wa mazingira tangu Mei, mwaka huu, ambapo aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola, alitembelea na kueleza kutoridhishwa kwake na hali ya uhifadhi wa mazingira.
Mambo yaliyoonekana kuwa ni tatizo ni pamoja na mabaki ya damu kwenye eneo hilo ambayo yalipelekea uwepo wa nzi wengi, kuziba kwa mitaro ya kupitisha maji machafu, kukosekana kwa utaratibu madhubuti wa kuhifadhi mbolea, kiwango duni cha shimo la kuhifadhia uchafu, harufu mbaya na ukosekanaji wa mpango endelevu.
Hivyo serikali kwa kuheshimu afya za wananchi na mazingira ki ujumla imeamua kukifungia kiwanda kwa sasa.
Na Bashiru Ally.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

NEMC YAFUNGIA KIWANDA CHA NYAMA YA PUNDA
Reviewed by By News Reporter
on
11/06/2018 06:50:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: