Loading...
Tafiti zimethibitisha taasisi na kampuni zinazoendeshwa na wanawake katika nafasi za juu za uongozi zimepata matokeo chanya, huku idadi ya wanaume kuongoza bodi mbalimbali za taasisi za Serikali ikipungua na wanawake wakiongezeka.
Mbali na hilo idadi ya majaji wanawake imeongezeka na kufikia 39 kati ya 95, ukilinganisha na 34 kati ya 97 mwaka 2012.
Hayo yamesemwa Jumatatu Novemba 18, 2018 na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa wanawake katika uongozi ulioandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (Ate).
Amesema kwa kulitambua hilo Serikali imeanzisha mpango mkakati wa kitaifa kwa ajili ya maendeleo ya usawa wa kijinsia uliopo kwenye dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025, kwenye lengo la kuwapo usawa wa wanawake na wanaume kwenye nyanja za uchumi, elimu, mafunzo na ajira.
Na Catherine Bulembo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

UTAFITI UMEBAINI MAKAMPUNI YANAYOONGOZWA NA WANAWAKE YANAFANYA VIZURI
Reviewed by By News Reporter
on
11/20/2018 08:22:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: