Loading...

WANAFUNZI TAKRIBANI 80 WATEKWA CAMEROON

Loading...
Wanafunzi karibu 80 na wafanyakazi wa shule wametekwa, kwenye mkoa unaozungumza kiingereza nchini Cameroon. Tukio hilo limetokea mnamo rais Paul Biya akitarajiwa kuapishwa tena kwa muhula wa saba madarakani.

Vyombo vya habari nchini humo vinataarifu kuwa wanafunzi hao waliotekwa usiku wa Jumapili, Novemba 4, walikuwa na umri kati ya 11 na 17 na walichukuliwa kutoka kijiji cha Nkwen kilicho karibu na mji wa Bamenda, sambamba na wafanyakazi akiwemo mkuu wa shule.

Msimamo wa serikali ya Cameroon ulitoa kauli kwamba haiwezi kurudi nyuma na watahakikisha watu wote pamoja na wanafunzi,  waliotekwa wanarejea katika madarasa na hatua kali zinachukuliwa na vikosi vya usalama kuhusiana na hilo - kauli iliyosema na gavana Deben Tchoffo.

Kwa mujibu wa kanda ya video iliyorushwa katika mitandao ya kijamii na kundi la Amba Boys ambao ndio washukiwa wakubwa wa tukio hilo. Wamedai kuwa wanataka kujitenga na kuanzisha nchi mpya ndio maana wamefanya hivyo.

Zahama hiyo nchini Cameroon inakuja baada ya rais Paul Biya kushinda uchaguzi mwezi uliopita kwa muhula wa saba na alitarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAFUNZI TAKRIBANI 80 WATEKWA CAMEROON WANAFUNZI TAKRIBANI 80 WATEKWA CAMEROON Reviewed by By News Reporter on 11/08/2018 07:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.