Loading...
Katika kijiji cha Nyamashekhe kilochopo mkoa wa magharibi nchini Rwanda kumekithiri utamaduni wa wanawake kulipa pesa kwa mwanaume ili waolewe.
Mtindo huo mpya wa maisha umezua gumzo katika jamii huku baadhi ya watu wakihoji hatima ya siku zijazo za utamaduni wa kulipa mahari.
Mtandao mmoja wa habari ulifika Kijijini hapo na kufanya mahojiano na wanakijiji kadhaa ili kujua undani wa swala hilo.
Kaitesi Lilian mmoja wa kina mama wa kijiji hicho alisema "Mvulana anapokuja kumposa msichana wako unajua kwamba mambo yameiva, lakini ndoa ikikaribia unasikia kwamba amemgeuka na kumwambia kwamba ndoa haitawezekana ikiwa hatapewa pesa za mahari".
Alipoulizawa mbona wanawake wengine wameolewa bila kufuata utaratibu huo alifafanua kwa kusema"Wakati huo binti alikuja na kuangua kilio huku akinishinikiza niuze kila kitu hata mabati au shamba ilimradi yeye apate pesa ya kumpa mchumba wake.
Tofauti na maeneo mengine ya nchi ambapo mwanaume ndio hutoa posa kwa familia ya mwanamke, utamaduni huu mpya unawashinikiza wasichana kumlipa pesa mwanamume.
Inasadikiwa kuwa pesa hizo ni kama dola 1500 sawa na Tsh3,600,000 na huongezeka kulingana na uwezo wa familia ya msichana.
Waliyoshuhudia wanasema pesa hizo lazima zipatikane kwa udi na uvumba.
Sababu kubwa ya vijana kufanya hivyo ni kuwa idadi ya wasichana imekuwa kubwa kulinganisha na idadi ya waoaji - kwa mujibu wa wanaume waliohojiwa.
Na Said Rajab.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WANAWAKE KUPOSA NA KULIPA MAHARI RWANDA
Reviewed by By News Reporter
on
11/07/2018 06:51:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: