Loading...

AFARIKI BAADA YA KUNG'OLEWA MENO YOTE

Loading...
Mwanamke mwenye ulemavu wa akili amefariki dunia baada ya meno yake yote kung'olewa katika hatua ambayo imekosolewa vikali nchini Uingereza.

Rachel Johnston, 49,  alifanyiwa oparesheni hiyo baada ya madaktari kubaini kuwa meno yake yote yameoza.

Lakini alizirai saa kadhaa baada ya kutolewa hospitali ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa.

Familia yake iliyokuwa imejawa na wasisiwasi ilifahamishwa kuwa madaktari hawakuwa na uwezo wa kuyaokoa maisha yake.

Upasuaji huo ulifanywa na wataalamu wa meno katika kituo cha afya cha Worcestershire.

Aidha, kitendo hicho cha Bi Johnston kung'olewa meno yote katika kituo cha afya cha Worcestershire kimezua utata ikiwa makundi ya kutetea haki yanasema kuwa kumekuwa na visa vya mgongano wa mawasiliano kati ya wagonjwa wenye ulemavu na familia zao, na kutoa wito kwa madktari wa meno kuingilia kati ili kuzuia visa vya mtu kung'olewa meno yote.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AFARIKI BAADA YA KUNG'OLEWA MENO YOTE AFARIKI BAADA YA KUNG'OLEWA MENO YOTE Reviewed by By News Reporter on 12/16/2018 09:44:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.