Loading...

BURUNDI KUBADILISHA MJI MKUU WAKE

Loading...
Sasa mji mkuu wa kisiasa nchini Burundi kuwa Gitega. Bujumbura ambao ndio ulikuwa mji mkuu wa kisiasa na kiuchumi hivi sasa kubaki na hadhi ya mji mkuu wa kiuchumi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jean-Claude Karerwa Ndenzako, msemaji wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter inasema baraza la mawaziri limeridhia kuanzia mwanzoni mwa mwaka mpya 2019, mji mkuu wa kisiasa uwe Gitega.

Mji mkuu wa sasa Bujumbura utabaki kuwa mji mkuu wa kiuchumi. Ndenzako alisema kuanzia mwanzoni mwa mwaka ujao vikao vya baraza la mawaziri vitafanyika Gitega na katika hatua ya mwanzo wizara 5 zitahamishia ofisi zake Gitega.

Bujumbura inapatikana mashariki mwa nchi ya Burundi pembezoni mwa ziwa Tanganyika na ina idadi ya watu milioni 1 na laki 2 wakati Gitega inapatikana katikati ya nchi ya Burundi na ina idadi ya watu laki 3.

Nkurunziza, mwaka 2007 alitoa ahadi ya kuifanya Gitega kuwa mji mkuu wa kisiasa wa Burundi.

Gitega, ulikuwa ndio mji mkuu kipindi cha utawala wa kifalme uliomalizika mwaka 1966.

Wapinzani wanamtuhumu rais Nkurunzinza ambaye amedumu madarakani kwa miaka 13 sasa kwamba anataka kurudisha utawala wa kifalme.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BURUNDI KUBADILISHA MJI MKUU WAKE BURUNDI KUBADILISHA MJI MKUU WAKE Reviewed by By News Reporter on 12/24/2018 10:02:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.