Loading...

WATAFITI WENGINE WALETA MATUMAINI MAPYA UGUNDUZI DAWA YA UKIMWI

Loading...
Wanasayansi wametoa hakikisho kuwa wanakaribia kupata tiba ya virusi vya HIV, hii ni baada ya kufanikiwa kupata dawa za kuuwa seli zilizoathirika na virusi hivyo.

Virusi hivyo hutibiwa kwa dawa za ARVs ila dawa hizo hazina uwezo wa kuondoa seli zilizoathirika mwilini.

Kulingana na ripoti iliyochapishwa na Daily Mail, watafiti katika taasisi ya Paris Pasteur walidai kuwa waliweza kuua seli zilizoathiriwa na virusi vya HIV mwilini.

"ARVs haziwezi kuondoa virusi hivyo mwilini. Tumeweza kuua seli zilizoathirika na kuziondoa mwilini," msemaji wa watafiti hao alisema

Utafiti huo ulifadhiliwa na Institute Pasteur, AmfAR (American Foundation for AIDS research) kSidaction.

Pia hapo hawali, watafiti kutoka Izrael walidaiwa kugundua dawa ambayo inaua virusi hivyo vya HIV kwa asilimia kubwa na bado wapo katika jaribio la mwisho ili kuwa na uhakika na jaribio lao.
Na Ummy Kitwana.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WATAFITI WENGINE WALETA MATUMAINI MAPYA UGUNDUZI DAWA YA UKIMWI WATAFITI WENGINE WALETA MATUMAINI MAPYA UGUNDUZI DAWA YA UKIMWI Reviewed by By News Reporter on 12/24/2018 08:56:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.