Loading...
PATASHIKA iliyosabishwa na mtokea benchi, Hassan Dilunga katika dakika ya 88, kwa kuambaa na mpira kisha kummegea pande Clatous Chama aliyefunga bao la tatu kwa ufundi wa hali ya juu akitumia kisigino, ndiyo iliyowahakikishia mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba bilioni 1.3 kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika, Caf.
Magoli mengine yalifungwa na Mkude, 29', Kagere, 45' + 1', na mabao hayo kuisababishia simba kupata ushindi mnyoofu uliowapereka hatua za makundi.
Kwa matokeo hayo sasa Simba inasubiri droo ya hatua ya makundi kujua wapinzani wake wa tatu ambapo hatua hiyo itachezwa kwa mtindo wa ligi nyumbani na ugenini na timu mbili zitakazoongoza kutoka kila kundi kati ya manne, zitatinga robo fainali.
Hivyo, kwa Simba tu kufuzu hatua hiyo, tayari ina uhakika wa kutia kibindoni Sh. bilioni 1.3 kutoka Caf, lakini kama itatinga hatua ya robo fainali italamba Sh. bilioni 1.5 wakati ikitwaa ubingwa Sh. bilioni 5.7 zitakuwa zinaihusu.
Na Hussein Masha.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

SIMBA YAJINYAKULIA BILIONI 1.3/- Caf
Reviewed by By News Reporter
on
12/24/2018 08:07:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/24/2018 08:07:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: