Loading...
Daktari aliyejulikana kwa jina Tobias Wara Obutu ambaye anafanya kazi katika eneo Nyatike, kaunti ya Migori, Kenya anazuiliwa na polisi baada ya kudaiwa kumbaka mmoja wa wagonjwa wake.
Mshukiwa alidaiwa kutoweka kusikojulikana baada ya kudaiwa kutekeleza kitendo hicho siku ya Jumatano terehe 27 Disemba, 2018 katika kituo chake cha afya kilichopo mjini Muhuru Bay.
Taarifa kutoka polisi zinaonyesha kuwa mwathirika ambaye jina lake halikuweza kutajwa alikwenda kwenye kliniki ya Frontal Medical ambapo mhudumu huyo wa afya alimpeleka kwenye chumba cha siri na kudaiwa kumchoma dawa za usingizi.
Mhudumu huyo alidaiwa kumbaka mwanamke huyo aliyelala kutokana na dawa alizopewa. Aliamua kutoroko baada ya kutekeleza kitendo hicho na kumwacha mwanamke huyo akiwa uchi na hana fahamu.
"Daktari huyo alimchunguza na kumwambia kuwa alihitaji damu zaidi. Alimpeleka kwenye chumba cha siri na kumchoma. Alipoteza fahamu kisha daktari huyo akambaka na kutoweka," Msemaji wa polisi wa Nyatike John Musili alisema.
Mwanamke huyo alipopata ufahamu alijikuta akiwa uchi. Alikimbizwa hospitalini ambapo alithibitishwa kubakwa.
Ripoti iliwasilishwa kwenye kituo cha polisi eneo hilo na kupelekea kukamatwa kwa mshukiwa huyo.
Daktari huyo wa afya atafikishwa mahakamani baada ya polisi kukamilisha uchunguzi.
Na Billy John.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

DAKTARI ANAYEDAIWA KUMBAKA MGONJWA ATIWA MBARONI
Reviewed by By News Reporter
on
12/30/2018 04:10:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/30/2018 04:10:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: