Loading...

ISRAEL KUJIANDAA NA VITA KUBWA KATIKA UKANDA BAADA YA MAREKANI KUFANYA MAAMUZI

Loading...
Baada ya Marekani kufikia uamuzi wa kuondoa jeshi lake nchini Syria habari zilizopo ni kwamba Israel inajiandaa na vita kubwa katika ukanda

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na gazeti la  Nezavisimaya la nchini Urusi, uamuzi wa Marekani kuondoa jeshi lake nchini Syria umepelekea kuilazimu Israel na jeshi lake  kupigana peke yake dhidi ya Iran.

Gazeti hilo la Urusi limeripoti kwamba waziri wa zamani wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman amesema kujiondoa kwa Marekani Syria kunasababisha uwepo wa uwezekano mkubwa wa mgogoro wa kivita kusini mwa Israel, Lebanon au nchini Syria.

Gazeti hilo pia lilimnukuu mtaalamu wa jeshi la Urusi Yuri Liamin, akisema kwamba uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kuiondoa Marekani nchini Syria usitafsiriwe kama ushindi kwa Iran. 

Rais wa Marekani, Trump wiki iliyopita alisema kwamba Marekani itaondoa askari wake nchini Syria.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
ISRAEL KUJIANDAA NA VITA KUBWA KATIKA UKANDA BAADA YA MAREKANI KUFANYA MAAMUZI ISRAEL KUJIANDAA NA VITA KUBWA KATIKA UKANDA BAADA YA MAREKANI KUFANYA MAAMUZI Reviewed by By News Reporter on 12/28/2018 09:57:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.