Loading...
SERIKALI imetoa sababu za kuzuia ndege mpya za Shirika la Fastjet kutua nchini kuwa ni kushindwa kutimiza masharti.
Imesema maneno ya Mkurugenzi wa Shirika hilo, Lawrence Masha, kwamba ndege hizo zimezuiwa kuingia nchini bila kuelezwa sababu si ya kweli.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga nchini (TCAA), Hamza Johari, alitoa ufafanuzi huo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema Desemba 24, Fastjet iliwasilisha ombi la kuleta ndege, lakini TCAA ilisema inalifanyia kazi ombi lao ili kuona kama wanastahili kuendelea.
Johari alisema si kweli kwamba ndege za shirika hilo zimezuiwa kuingia bila maelezo kama alivyosema Masha, bali walimweleza kwamba anapaswa kukamilisha masharti ya kuendesha biashara hiyo. Ikiwa ni pamoja na kulipa deni lote la kiasi cha Sh. bilioni 1.1 walizokuwa wanadaiwa na mamlaka hiyo, ambapo mpaka sasa wamelipa kiasi cha Sh. milioni 800 pekee.
Hivyo mamlaka imewapa notisi na wamefanikiwa kulipa kiasi cha fedha za madeni, lakini wanapaswa kuyalipa na mashirika mengine kama Swisport, TAAA na Cadco ambayo yanawadai Sh. bilioni 5.2.
Na Lawrence John.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

SABABU ILIYOWAFANYA FASTJET KUZUILIWA KUTUA NCHINI
Reviewed by By News Reporter
on
12/28/2018 09:26:00 AM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/28/2018 09:26:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: