Loading...

KATIKA MAPUNGUFU ULIYONAYO WEWE BADO WA THAMANI

Loading...
Ukweli ni kwamba pamoja na mapungufu ama madhaifu uliyonayo bado wewe una thamani ya kipekee na tofauti na wengine. Hebu jithamini na kujikubali kwa namna ya jinsi ulivyo hivyo hivyo katika hali hiyo hiyo ya mapungufu.

Ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufanikiwa katika maisha yako ni lazima kwanza ujitambua jinsi ulivyo, ujikubali jinsi ulivyo na uthamini utofauti wako na wengine kimapungufu na uwezo. Kufanya hivyo ni fursa ya wewe kuweza kutafuta suluhu ya mapungufu yako na kuyashughulikia.

Watu wengi wanatumia nguvu nyingi kuficha uhalisia wao kwa kuvaa ubandia ili kuficha mapungufu waliyonayo, kumbuka hii inasababisha kukuletea watu ama marafiki ambao ni tofauti na wewe ulivyo. Hawa hawatakuwa na msaada sana kwako kwa sababu pindi watakapobaini uhalisia wako wataondoka.

Kukubali mapungufu uliyonayo na kuishi katika uhalisia inakusaidia kutafuta njia za kuondoa madhaifu hayo na pia kukukutanisha na watu sahihi ambao watakukubali katika hali yako na kukusaidia kutatua mapungufu uliyonayo.
Na Saidi Juma.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KATIKA MAPUNGUFU ULIYONAYO WEWE BADO WA THAMANI KATIKA MAPUNGUFU ULIYONAYO WEWE BADO WA THAMANI Reviewed by By News Reporter on 12/28/2018 08:37:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.