Loading...
Jaji Mkuu David Maraga na mkewe wamefikishwa katika hospitali ya War Memorial iliyopo Nakuru baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya barabara kuu ya Nakuru - Eldoret.
Katika taarifa ya JM, ilisema: Mke wangu na mimi tumepata ajali maeneo ya Nakuru asubuhi ya leo tukielekea Kanisani. Tunafanyiwa uchunguzi na madaktari. Dereva wangu na kijakazi wapo salama. Tunamshukuru Mungu kwa miujiza yake. Asanteni Wakenya kwa maombi yenu na kuguswa.
Rais Uhuru ameagiza jeshi kumpatia Jaji Mkuu pamoja na mkewe Yucabeth Nyaboke usafiri wa dharura ili waperekwe mjini Nairobi kwa matibabu zaidi.
Taarifa kutoka hospitalini zinasema Jaji Mkuu ameumia sehemu za kichwani na Mkewe alipata mshtuko lakini anaendelea vizuri.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

JAJI MKUU 'DAVID MARAGA' NA MKEWE WAPATA AJALI MBAYA - KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
12/22/2018 02:02:00 PM
Rating:
Reviewed by By News Reporter
on
12/22/2018 02:02:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: