Loading...

KIKWETE ALINIAMBIA NIOE MUDA UMEFIKA, ALINIPA POLE:- DIAMOND PLATINUMZ

Loading...
Msanii mkubwa Tanzania na Afrika ki ujumla amefunguka na kuelezea kwa undani juu ya mkutano wake aliokutana na mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete wiki iliyopita mabapo picha nyingi sana zilisambaa katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha akiwa na kiongozi huyo.

Hata hivyo Diamond anasema kuwa kabla ya kwenda kumuona , aliongea nae kwenye simu na kumtaka wakutane ili kumpa pole kutokana na ajali aliyokuwa ameipata akiwa sumbawanga.

"Nilipokuwa Mwanza , niliambiwa kuwa amekuwa akinitafuta hivyo niliamua kumpigia na kuongea nae, aliniliuza kama kweli nimedondoka na nikamuelezea jinsi situation ilivyokuwa na kwa sababu hatukuwa tumeonana siku nyingi sana nikamwambia kuwa nikirudi dar ntakuja kukuona baba.

"nilivyorudi nikaenda kuonana nae na aliniambia mambo mengi lakini alisema nioe muda wa kuoa umefika sasa, kuna clip moja  aliona tulikuwa tunahesabu ela na tanasha akaniambia kuwa sio vizuri kuna watu hawana hata riziki kwahiyo wakiona wanakuwa wanajisikia vibaya," alisimulia Diamond Platinumz.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KIKWETE ALINIAMBIA NIOE MUDA UMEFIKA, ALINIPA POLE:- DIAMOND PLATINUMZ KIKWETE ALINIAMBIA NIOE MUDA UMEFIKA, ALINIPA POLE:- DIAMOND PLATINUMZ Reviewed by By News Reporter on 12/27/2018 04:06:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.